| KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA GEITA KAMISHINA MSAIDIZI JOSEPH KONYO AKIONYESHA BUNDUKI AINA YA SMG ILIYOKUWA INATUMIWA NA MAJAMBAZI JANA |
Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha ya
bunduki aina ya SMG na bastola waliokuwa wakitumia pikipiki aina ya
sanlg yenye namba T460 CVQ wamevamia duka la mpesa na kumuua
mfanyabiashara Gosbert Kulwa(59) mkazi wa tambukaleli mjini Geita.
Kamanda
wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo amesema tukio hilo limetokea jana
majira ya saa 11.30 jioni katika eneo la benki ya NMB ambapo majambazi
hao walimpiga risasi ya tumboni mfanyabiashara huyo wa mpesa na kufariki
dunia wakati akipata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Geita.
Amesema
mauaji hayo yalifanyika baada ya majambazi hao kupora kiasi cha pesa
ambacho hakijajulikana kutoka kwa mfanyabiashara huyo.
Kamanda
ameongeza kuwa kabla hawajamuua Gosbert walianzia kwenye duka la
mfanyabiashara wa vinywaji ndugu Ignas Athanas na walichukua pesa kiasi
ambacho hakijafahamika na kuchukua bastola aina ya H PIETRO BERRETA HO4788Y CAR 5808 ikiwa na risasi 12 mali ya mfanyabiashara huyo.
Aidha majambazi hao waliokuwa na bunduki aina ya SMG iliyofutwa namba zake na risasi 13 na simu ya mkononi aina ya TECNO huku wakiwa wamevalia makoti meusi na helment ili kuficha sura zao zisitambulike kwa urahisi.
Jeshi
la polisi lilipata taarifa muda mfupi zilizotolewa na raia wema ambapo
kamanda wa polisi akiongoza kuwafuatilia majambazi hao walifanikiwa
kuwakuta katika pori lililopo jirani na kijiji cha Ibambila wilayani
Nyangh’hwale zaidi ya km 50 kutoka mjini Geita walipofanya uharifu.







Post a Comment