VAI WA UKWELI NUSURA AVUNJE MGUU!


Na Hamida Hassan
MUIGIZAJI wa filamu Bongo Movies, Isabela Francis ’Vai wa Ukweli’ nusura avunje mguu chumbani kwake baada ya bwana’ake Boniface kuibukia uvunguni mwa kitanda ghafla.
Muigizaji wa filamu Bongo, Isabela Francis ’Vai wa Ukweli’.
Akipiga stori na Amani, Vai alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo pasipo kujua lengo lake, mchumba wake huyo alijificha uvunguni kama mtu aliyekuwa anamtegea kitu alipoona mtego haujafanikiwa akaibuka.
“Nilitoka na yeye akatoka sasa niliporudi niliongozana na rafiki yangu mmoja wa kike na kuna washikaji zetu walikuja kututembelea tukiwa tumeshakaa sana tukashangaa mtu anatokea uvunguni mwa kitanda, nilishtuka na kuruka nusura nivunjike mguu,” alisema Vai.
Vai aliongeza kuwa, kuanzia siku hiyo akiingia ndani kabla ya kufanya chochote lazima aangalie kila kona ya chumba chake

This entry was posted in